Msanii AT kutoka Tanzania

Hivi karibuni kumeibuka mrushiano wa maneno kati ya wasanii wawili kwenye bongofleva ambao ni Msami na AT ambapo ilianzia kwa AT kuulizwa kwenye interview akasema hamjui Msami.
 
Baada ya maneno hayo Msami alipost video kwenye Instagram yake na kumwambia AT kwamba anamshukuru kwa kumuita mcheza mpira, "Mimi najua unanijua ndani ya nafsi yako, mimi sina tatizo na wewe, kwenye dunia ya sasa unatakiwa kukubali kwamba lazima tupokezane kijiti, mimi nilikua dancer na ilitakiwa nitoke wabaki watu wengine."
 
Mbali na mrushiano huu wa maneno, kutana na Msami na AT na muziki yao kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)
 
Baada ya maneno hayo, AT ameongea na DStv na kueleza yafuatayo, "Kuna tofauti kati ya kumjua na kumfahamu, ukishindwa kujua kiswahili utakosana na mimi lakini najua kwa kuona kuwa huyu ni Msami.... kikubwa kuna mahali atakua kateleza."
 
Aliendelea, "Ni muda mrefu amekua na chokochoko na mimi kwamba aliniona na mwanamke, sijui ni Uwoya..... mimi siwezi kugombania Mwanamke na Msami, kama ni Irene Uwoya yule nishabiki yangu mkubwa tena shabiki haswa."
 
AT alimalizia, "Msami anaweza kunishinda kucheza kwenye stage lakini sio vitu vingine, tukiingia studio mimi namkalisha.... asishindane na mimi, yeye bado ni msanii ambaye hajawahi kumiliki tuzo hata ya mbao ya kuchonga mwenyewe."