Msanii Msami kutoka Tanzania

DStv.com inae mwalimu wa dancers na msanii wa bongo fleva Msami ambapo kitu kimemleta kwenye hii post ni kuhusiana na yeye kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Irene Uwoya.

Kutana na Msami kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo (160).

Iliripotiwa kuwa wawili hao, Msami pamoja na Irene Uwoya kuwa katika mahusiano lakini Uwoya alitoa usemi na kufunguka kuwa wameshaachana.

Namnukuu Msami akisema, "Kuachana kama kuachana me siwezi kuizungumzia kama tumeachana ila mimi niliamua tu nikae pembeni’

Msanii huyu aliendelea kusema kuwa aliamua kusogea pembeni tu bila sababu yeyote ila nikwamba tu watu wana complicate swala hilo lakini sio kubwa wala hawakuwa na ugomvi wowote.

Msami alisisitiza, "Tunacommunicate kama washkaji tu freshi yani, ila ukiniuliza sababu katika swala la kuachana naikosa kwasababu nilikaa tu siku nikasema no sitaki iwe hivi nataka iwe hivi."