Msanii Mr Nice

DStv.com inae msanii kutoka Tanzania Mr. Nice ambaye ameongelea swala la kurudi tena kwenye mziki baada ya ukimya wa mda mrefu .

Msanii huyu Lucas Mkenda anayefahamika kama Mr.Nice amekuwa na ukimya wa muda mrefu sana na kufanya washabiki kujua kashatoka kwenye game licha ya yeye kufanya muziki wa gospel mara ya mwisho lakini amevunja ukimya na kusema kuhusu ujio wake mpya.

Kwenye exclusive hii Mr.Nice ameelezea, "Kuna ujio mpya unakuja hivi karibuni na ni mzuri sana, unajua watu wazima hatuna haraka tunafanyaga mambo polepole that’s why tumeitwa wakongwe coz tunafanya mambo kwa uwakika na sio kwa kubahatisha."

Mr.Nice amesema pia anakuja kwa kasi na watu wategemee surprise ambayo kuna collabo anategemea kufanya na msanii kutoka Kenya na ni msanii wa sasa na anafanya vizuri pia kwenye muziki.

Mr.Nice alimalizia kwa kusema, "Sasa hii nikwamba pia kuna collabo ipo jikoni na naifanya na Jaguar tunangalia jinsi gani tunaifanya ili tufanye mambo ambayo yako katika hadhi yetu kwasababu kama wewe ni mkongwe unatakiwa utendee ukongwe wako haki."

Colabo hii mpya basi kwa hakika utaipata kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.