Msanii wa Nigeria Mr Flavour

Flavour agusia kuwa kafanya collabo ingine na Diamond Platnumz

Sio kitu kipya sasa kuona kolabo ya Diamond na Mr Flavour wa Nigeria 'Nana' ikipigwa zaidi ya mara mbili kwa siku moja katika TV Stations kubwa kama TRACE Urban na MTV Base, kwa wale wenye ving'amuzi vya DStv.

Burudika na hit single hii ya Nana na mengine mengi kwenye Base Lines Jumamosi saa 17:00 kwenye MTV Base.

Ni kutokana na ukali ambao wawili hawa wameuonyesha kwenye hii kolabo ambayo ilirekodiwa au ilianza kufanyiwa kazi toka mwaka 2014.
 
Ni wimbo wa Diamond Platnumz lakini good news ya leo ni kutoka kwa Mr. Flavour ambae anasema soon tu itakua zamu yake kuachia wimbo aliofanya na Diamond Platnumz.
 
Flavour ambaye alikua miongoni mwa wasanii waliopamba tamasha la MultiChoice nchini Mauritius lililoandaliwa kwa waandishi na watangazaji wa Afrika kuonyesha vitu mbalimbali zikiwemo bidhaa mpya za DStv, amesema amezingatia kolabo na Diamond sababu anajua nguvu yake.
 
Kwenye exclusive na dstv.com, Flavour hajapenda kusema ni lini hii kolabo itatoka ila kathibitisha kwamba itakua kwenye audio pamoja na video na anaamini kwa kupitia Diamond atawafikia watu wengi sana kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
 
Flavour anasema toka alipokutana na Diamond kwa mara ya kwanza ameonyesha ni kijana mnyenyekevu, hana maringo na amekua serious na kazi kiasi kwamba inampa moyo na imemuonyesha ni mtu wa aina gani.