Msanii wa bongofleva Mr Blue wa Tanzania

Mr Blue aongelea kuhusu Baraka the Prince kwenye exclusive

DStv.com inae msanii wa bongofleva Mr. Blue kwenye hii post ambapo kitu ambacho kimemleta kwenye hii post ni kuhusu ishu yake ya malumbano na mwimbaji wa bongofleva Baraka the Prince.

Iliripotiwa kwamba wawili hawa walitofautiana au walipishana baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao kwamba Mr. Blue amempigia simu saa nane usiku mpenzi wa Baraka aitwae Naj, ambaye ni girlfriend wa zamani wa Mr. Blue.

Kutana na Mr Blue na pia Baraka the Prince kwa chaneli mpya, TRACE Mziki itakayoanza siku ya Alhamisi, 1 September (channel 323).

Blue amesema weekend iliyopita ilibidi amfate Baraka uso kwa uso wakiwa Mwanza kwenye Fiesta ili ajue nini tatizo ambapo anasema baada ya kukaa akaelewa kwamba Baraka sio mtu mbaya na kwamba vinavyosambazwa dhidi yao vinatengenezwa na watu wengine.

Kwenye exclusive na DStv, Blue amesema wameshamalizana na Baraka na sasa hivi wako kwenye hali nzuri na wanaongea, hakuna tena ugomvi na anamuheshimu kama mdogo wake.

Namnukuu Blue akisema: “Baraka ni mdogo wangu na nitaendelea kumuheshimu kama mdogo wangu, napenda muziki wake na toka kitambo mimi ni shabiki wa muziki wake... ana muziki mkubwa sana na hatakiwi kuzingatia au kujihusisha na hizi skendoskendo.”