Msanii Mr Blue kutoka Tanzania

Unajua kwamba Mr. Blue alikua akiumiza kichwa atapata wapi pesa za kumalizia nyumba yake mwaka juzi na hakujua atazipata wapi milioni 40?

Kwenye msimu huu wa tamasha la FIESTA Mr. Blue amekumbuka mengi na kuongea kwa mara ya kwanza kwamba tamasha la FIESTA mwaka juzi lilimpa zaidi ya milioni 40 alizokua anahitaji kumalizia nyumba yake.
 
Msanii huyu Mr. Blue anakujia kwenye Mziki Fresh, Jumatatu hadi Ijumaa saa 20:00 kwenye channel mpya ya TRACE Mziki (323).
 
Blue ambae yupo pia kwenye list ya wakali wa mwaka huu pia amesema: "Time ile mambo hayakua mambo mazuri kabisa kwangu, malipo ya fiesta yalinifanya nimalize nyumba na kuweka kila kitu na ndio nyumba ambayo naishi."
 
"Nilikua naishi maisha ya tabu kabla ya hapo, nilikua nakaa chini na kwenye nyumba ambayo haina umeme ila baada ya kulipwa kwenye fiesta ndio nikaweka kila kitu, siwezi kuwa mnafiki fiesta ilinitoa kwenye giza na kuniweka kwenye mwanga," kasema Mr. Blue.
 
Mr Blue kwa kumalizia anasema pesa aliyoipata fiestani pia aliweza kununua gari na bado nyingine ikabaki, ndio maana hata kama hatoalikwa kwenye fiesta tena bado upendo wake kwa fiesta utabaki palepale.