Meneja Mkubwa Fela

Kutana na Said Fela mkimfahamu kama Mkubwa Fela au Mkubwa na anae anaeimiliki Yamoto Band lakini pia ni mananger wa wasanii kama Diamond Platnumz, Chegge Chigunda na Temba.

 
Kumekuwa  na headlines za Said Fela kuanza kusimamia mziki wa taarab  na ndio sababu DStv.com ikabidi imsogeze karibu meneja huyo na kumuuliza taarifa hizo kama ni za kweli au na haya ndio yalikuwa maneno yake.

"Ni kweli naanza kusimamia mziki wa Taarab unajua walinifata baadhi ya wasanii wa Jahazi wakaniomba niwasimamie kutoka na kiongozi wa Band ile ya Jahazi mzee Yusuph ambae ameamua kumrudia Mungu na kuuanza kuimba nyimbo  za dini na kuachana na muziki wa dunia."

Aliongezea, "'Mimi nimekaa nikawaza nikaona ni sawa na nimeamua kuwasimamia kwa sababu wote wanategemea muziki kwa ajili ya kuendesha maisha yao na jina la Band itaitwa Ya TMK Morden Taarab."

Kwa muziki za kiasilia za Kitanzania, usikose kutazama Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.