Mtanzania Shilole

"Mpaka hapa nilipofikia nina uwezo wa kujiita malkia wa nguvu," Shilole amesema.
 
Shilole alianza kufahamika baada ya kuingia kwenye tasnia ya uigizaji kwenye bongo movies Tanzania lakini jina lake lilizidi kufahamika baada ya kuingia rasmi kwenye bongofleva.
 
Tazama bongo movie Zinda siku ya Ijumaa 31 March saa 20:00 kwenye Maisha Magic Bongo (160).
 
Shilole amekuwa akifanya mziki wa aina yake na utofauti katika mziki wake ndo umepelekea kupata mashabiki wengi na shangwe kubwa anapokuwa kwenye stage.
 
Muziki umempatia shilole jina lakini pia maendeleo, ambapo ameweza kufungua biashara ya chakula aliyoipa jina la Shishi Trump Food Delivery ambayo kwenye hiyo biashara Shilole anapika vyakula vya kiafrika kama ugali, samaki, wali, pilau, ndizi na vingine vingi.
 
Kupitia kampeni ya Malkia wa Nguvu iliyoanzishwa na kampuni ya Clouds Media Group kwa lengo la kutambua umuhimu wa mwanamke na jitihada za kuwainua wanawake, Shilole alisema kwa kiwango alichofikia akilinganisha na alipotokea anaweza kujiita mwanamke wa nguvu.
 
"Nilianza sikuwa na uwezo nikaona niingie bongomovie baadae niona naweza kufanya muziki na utaniongezea kipato, leo hii ninamiliki mgahawa wa chakula ukiangalia safari yangu kuanzia nilipotoka mpaka nimefika hapa aisee mimi ni Malkia wa nguvu bwana," Shilole alisema.