Model wa Tanzania Millen Magese

Pata kujua vile Millen anajisikia kuhusu tuzo maalum ya BET

Millen Magese ni miongoni mwa Watanzania ambao wamelifanya nchi ya Tanzania kutajwa sana kwenye matukio na hata habari kubwa kubwa.

Ni mwanamitindo ambaye headlines zake zimekua New York na Johannesburg ambako anafanya kazi hiyo kwa miaka mingi na yenye mafanikio pia.

Baada ya kutangazwa kama mshindi wa tuzo maalum ya kituo cha TV cha Marekani BET, Millen ameongea na dstv.com na kusema alishtushwa sana na taarifa hizo, ni taarifa ambazo hakuzitarajia wala hata hajawahi kuwazia.

Usisahau kutazama BET Awards 2015 itakayoonyeshwa kwenye BET (129) and BET2 (135) saa 20:10 CAT, Jumanne 30 June.

Amesema haya, "Nadhani sababu kubwa ya mimi kupewa hii tuzo ya heshima ni sababu nilijitokeza hadharani kwamba ni mgumba, haya ni mambo ya ndani ya mtu lakini mimi nilitoka hadharani nikijua nitawasaidia wengine wengi pia."

Sifa nyingine aliyo nayo Millen ni kwamba ni miongoni mwa watu maarufu wa Tanzania ambao hutoa misaada bila kutangaza kokote, yani amekua akifanya kazi nyingi za kijamii lakini hazitangazi, hiyo ni aina ya moyo wake.