Msanii Emmanuel Mbasha

Msanii wa injili Emmanuel Mbasha aachwa huru na mahakama

Jumatatu September 21 mahakama ilimwachia huru mwimbaji wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha aliyekua akikabiliwa na kesi ya ubakaji.

Ni kesi ambayo imetembea kwa miezi huku Emmanuel akiwa kwenye wakati mgumu wa kukabiliana na tuhuma nzito za ubakaji kwa shemeji yake ambaye ni mdogo wa Flora Mbasha.

Wanandoa hawa wawili waliacha kuishi pamoja muda mfupi tu baada ya kesi kuanza huku Flora akikiri kuhuzunishwa na kitendo cha mumewe. 

Mengi kuhusu ndoa, usikose kutazama kipindi cha Talaaka kila siku itakapoanza kwenye chanel mpya ya Maisha Magic Bongo kutoka tarehe 1 October.

Baada ya mahakama kuona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha ilimuachia huru Emmanuel Mbasha.

Hata hivyo pamoja na kuandamwa na kesi hiyo, Mbasha kwenye wiki kadhaa kabla ya kuachiwa huru aliongea na dstv.com na kusema alikua tayari kurudiana na mke wake na wala hakuwa tayari kumpa talaka.

Saa kadhaa kabla ya Hukumu kutolewa Mbasha alipost picha Instagram akionekana analia na kuomba watu wamuombee kwa Mungu.