Mshindi wa Airtel Trace Music competition Mayunga

Mshindi wa Airtel Trace Music Star Mayunga ajiandaa kufanya kazi na Akon

Mtanzania Mayunga ambaye alishinda kwenye Airtel Trace Music Star competition lililokuwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali Afrika yuko kwenye hatua za mwisho kuondoka bongo.

Shindano lenyewe lilikua na nchi 13 za Afrika zilizoshiriki ambapo miongoni mwa majaji alikuwepo Akon ambaye studio yake itatumika kufanya kazi na Mayunga kwa ajili ya kuirekodi hiyo single ya kwanza.

Burudika na muziki wa wasanii wa Kiafrika kwenye kipindi cha Official African Chart kila Jumanne saa 21:00 kwenye MTV Base. 

Huenda Mayunga akawa kwenye mikono ya Akon kwa muda mrefu sababu aliahidi kwamba kama single ya kwanza itafanya vizuri basi atampa dili la kufanya album.

 Haijawekwa wazi mpaka sasa kama Mayunga ataunganishiwa kolabo na mkali yeyote mwingine wa muziki kutoka Marekani lakini ishu kamili ni kwamba mpango lazima ukamilike kwenye muda uliopangwa na sasa ndio anafanya maandalizi ya mwisho ya kuondoka bongo kumfuata Akon.