Msanii Mayunga kutoka Tanzania, mshindi wa Airtel Trace Music Star Competition

Mayunga afunguka juu ya muda alitumia kutengeneza collabo na Akon

Staa wako mshindi wa Airtel Trace Music Star, Mayunga ambae amehit na song yake aliyorecord na msanii kutoka Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon iliyobeba jina Please Don't Go Away.

Kutana na Mayunga na wimbo wake kwenye Mziki Hit 30 Jumamosi saa 10:00 kwenye TRACE Mziki (323).
 
Amedondoka leo kwenye DStv.com ambapo ametueleza ni muda gani ametumia kufanya collabo yake na Akon.
 
Mayunga alisema, "Kwa kweli ningependa niweke tu wazi watu wafahamu me nimeenda kule Marekani for only one week u know. Na cha kwanza kabisa me kuulizia ilikuwa ni wimbo nikawaambia yani kama wimbo uko tayari yani nileteeni tu me nianze kuukariri mapema niushike lakini wakawa wananiambia nitulie."
 
Mayunga alimalizia, "Uwezi amini nilipewa wimbo leo kesho mchana unahitajika kurecord na niliumasta vizuri tu na kesho yake tukaingia studio na tukarecord bila tabu."