Mshindi wa Airtel Trace Mayunga na Akon

DStv yakutana na mshindi wa Trace Music Star competition ambaye afafanua kwa nini hajaanza kufanya collabo na Akon

Ni post maalum inayomuhusu Mtanzania Mayunga ambaye alishinda shindano la kusaka vipaji la vijana wa Afrika lililojumuisha nchi zaidi ya 10 huku miongoni mwa majaji akiwa ni Akon.

Mayunga aliposhinda kwenye Airtel Trace Music Star 2015 ilikua inatakiwa afanye kolabo na Akon huko Marekani, ndio mkataba ulivyokua unasema lakini mpaka sasa hajafanya kolabo na Akon licha ya kwanza ametoa single yake ya kwanza Nice Couple baada ya ushindi huo.

Pata kuburudika na Nice Couple ambayo sasa inachezwa kwenye TRACE Urban (DStv channel 325). 

Ameongea kwenye exclusive interview na dstv.com na kusema, "Hiyo ni kwa sababu Akon ana project ya mambo ya umeme Afrika, kilichofuata ni yeye kuendelea na project yake akishamaliza ndio tutaungana."

"Nimemuelewa na project yake na ndio maana namsubiria ila nikaona ni bora mi niendelee kutoa single tu, akishakua tayari nitaungana nae... vilevile mkataba wangu ni yeye kufanya ngoma moja na mimi kisha mimi nitaendelea kutoa zangu kivyangu labda kama yeye atapendelea kufanya kazi tena na mimi ila hakijaharibika kitu," kaongezea Mayunga.