Akon na mshindi wa Airtel Star Compettion Nalimi Mayunga

Mshindi wa Airtel Trace Music Star competition amemalizana na Akon baada ya kurekodi kolabo ya wimbo pamoja na video.

Mwimbaji Mtanzania Nalimi Mayunga ambaye alishinda kwenye shindano la Airtel Trace Music Star ambalo lilikua likitafuta mshindi mwenye kipaji cha kuimba kwa uwezo wa hali ya juu kutoka kwenye nchi kumi za Afrika, amemalizana na Akon

Moja ya zawadi za ushindi huo ilikua ni mkataba wa milioni 900 zilizotengwa maalum kwa ajili ya kurekodi single moja na video nchini Marekani, kolabo ambayo ni lazima alikua ashirikiane na Akon.

Itazame kipindi cha Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ili uweze kuburudika na kolabo zingine kutoka Tanzania na pia Afrika Mashariki.

Kwenye exclusive na DStv.com, Mayunga amethibitisha kwamba wameshamalizana na Akon kwenye kurekodi hiyo kolabo nchini Marekani alikokwenda 16 November, na wamesharekodi wimbo tayari na video ndani ya wiki moja.
 
Anasema, "Ni wimbo ambao unahusu mapenzi, kiukweli mimi mwenyewe niliposikilizishwa ule wimbo nilidata, ni wimbo ambao sijauandika mimi wala kutengeneza chochote kama melody, nilikuta tu wameshaandika na kunitengenezea kila kitu kazi ikabaki mimi kupita tu."
 
Kwa kumalizia, Mayunga amesema tarehe ya kutoka kwa hiyo single itatangazwa hivi karibuni na kwamba kingine cha kumfurahisha ni kwamba Akon amefurahi sana jinsi Mayunga alivyoimba. Akaongezea kuwa alipofika nyumbani kwake siku ya kwanza huko Los Angeles, Akon alimkaribisha na chakula cha mchana kwanza wakala ndio kazi ikaanza hivyo amekua mtu poa sana kwake.