Mayunga in Hollywood L.A

Mayunga yupo US kufanya kollabo na Akon

Mwimbaji mshindi wa shindano la Trace Music Star 2015 Mtanzania Mayunga ameshafika L.A Marekani tayari kurekodi na Akon.

Safari yake ni kutimiza ahadi ambayo iliyolewa kwa mshindi wa shindano hilo lililojumuisha washiriki kutoka nchi zaidi ya kumi Afrika.

Kwa mziki rasmi, tazama kipindi cha Mzooka kila siku saa 16:00 hapo Maisha Magic Bongo (160)

Kilichompeleka Mayunga Marekani ni kurekodi wimbo pamoja na video kwa kumshirikisha mwimbaji staa Akon.

 

 

Mayunga ameongea na DStv.com akiwa Marekani na kusema Ijumaa ya November 20, 2015 ndio alitarajiwa kukutana na Akon.

Atachukua muda wa wiki moja tu kupewa mafunzo, kurekodi wimbo pamoja na video yake kisha atarudi Tanzania.
 

Related