Msanii Maua Sama

Mwimbaji wa bongofleva Maua Sama asema kwenye exclusive kwamba hatosahau wazazi wake kwenye maisha yake kwa sababu baado wanamuangalia

Leo kwenye ripoti za DStv.com tunae mwimbaji wa bongofleva Maua Sama ambaye sasa hivi anayo hit single iliyoshika namba mbili wiki iliyopita kwenye CloudsFM Top 20 Mahaba Niue.

Kama kuna vitu Maua Sama hatovisahau kwenye maisha yake ni hii ya wazazi wake, bado ni mtoto wa nyumbani ambaye baba na mama wamekua wakimuangalia sana.

Mengi kuhusu maisha za kinyumbani, tabia njema na desturi za wanawake, ungana na Bi Mariam Wamigomba kwenye Mchichiko wa Pwani kila Jumatano saa 19:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Mwaka 2015 wazazi wa Maua walilazimika kuomba ruhusa kazini kwao ili tu kumpeleka mtoto wao kwenye show ya Tanga, yani wakaendesha gari wakiwa na Maua mpaka Tanga, wakasubiria akamaliza kuimba alafu wakarudi nae nyumbani Moshi.

Maua anasema haikua sababu hawamuamini au wanamchunga bali anaamini ile ilikua support tu, yani walitaka kuhakikisha yuko salama na kwenye show walihudhuria... alipomaliza kuimba wakarudi hotelini.

 

A photo posted by Maua Sama (@mauasama) on Jan 31, 2016 at 3:03am PST

Maua Sama ameshamaliza chuo na alikua akisoma kwenye chuo ambacho baba yake anafundisha Kilimanjaro, japo alikua anakaa hostel aliweza kutoroka mara kadhaa na kwenda Dar es salaam bila baba yake kujua.

Kwa sasa Maua amemaliza shule na amehamia Dar es salaam tayari kwa kuwa na full time kwenye muziki wake.

Mbali na Mchichiko wa Pwani, pia unaweza kuitazama DStv Catch Up ambayo inayo burudani tele kwenye DStv Explora. Jaza fomu hii kupata Explora yako kwa urahisi:

 

Fill out my online form.