Mwigizaji bongowood Vincent Kigosi

Vincent Kigosi adakua mambo matano ambayo labda hujui kumhusu yeye.

Leo ripota wako wa DStv Tanzania Millard Ayo anakukutanisha na kauli tano exclusive kutoka kwa mwigizaji Ray Vicent Kigosi.

Kabla ya hayo, ungana na Vincent Kigosi kwenye bongomovie ya Hard Price na filamu zingine zitakazoonyeshwa Jumatatu hadi Ijumaa saa 17:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

1. Sijawahi kupeleka movie zangu zikaonyeshwe kwenye majumba ya cinema sababu ya vikwazo kadhaa lakini huwa nakwenda cinema kutazama wengine.
 
2. Naishukuru sana DStv manake mafanikio ni makubwa ambayo nimeyapata kupitia hiyohiyo DStv, nilishawahi kupata mwaliko wa kwenda kuigiza movie Nigeria na marehemu Kanumba, japo haikufanikiwa lakini wamenikutanisha na vitu vingi.
 
3. Niligundua sinema zangu zikionyeshwa DStv napata kazi au kualikwa kwenye nchi kama Kenya, DRC, Burundi, Rwanda na sehemu nyingine, ni sehemu ambayo watu wengi wanaitazama hivyo inatupa soko kiukweli.
 
4. Mwigizaji wangu namba moja duniani ni Denzel Washington.
 
5. Nikiwa natazama movie nyingine huwa napenda sana za Afrika manake ni mazingira ambayo hata sisi tunayo, kuangalia zile movie za watu wanaruka kwenye magorofa hainisaidii kuliko ningeangalia movie za Afrika.