Mwanamitindo Rosemary Kokuhilwa

Kutana na Mtanzania Rosemary Kokuhilwa, Mwanamitindo aliyehamishia makazi yake New York kutokea Tanzania kwa miaka sasa hivi akiwa anaishi na kufanya maisha yake kutokana na uanamitindo.

Pia kutana na wanamitindo wengine kule New York kama EJ Johnson katika kipindi cha EJ NYC, Jumamosi saa 14:25 kwenye E! Entertainment (124).

Kuna vitu vingi vya kujifunza kwenye safari yake ya uanamitindo na mpaka kufika alipofika kuanzia alipofika mara ya kwanza Marekani na kuingia kwenye shule ya mambo ya fashion.

1. Nilikuja Marekani kusomea computer science lakini nilivyofika hapa nikajikuta napenda sana mambo ya fashion nikaamua kuifata na kuachana na mengine.
 
2. Kwa nchi ya Marekani kiwanda cha fashion ni kikubwa sana na kimepewa nafasi sana, niliamua kuingia darasani na kujilipia... kiukweli kupitia shule nimekutana na watu wengi sana mpaka leo.
 
3. Ada niliyolipa ni kubwa sana lakini shule imenikutanisha na watu wengi sana mpaka leo na kama isingekua wao ingeakua ngumu kufika hapa.
 
4. Nilisoma chuo cha fashion kwa miaka miwili, kiasi cha ada kwenye shule za fashion unachoweza kulipa kinafikia mpaka milioni 80 za Kitanzania kama ukitaka kumaliza vitu vingi.
 

5. Ilibidi nifanye kazi kwa bidii ili nipate pesa ya kujilipia ada, nilikua nafanya kazi za kijamii kuwahudumia watu waliopata ajali ambao wanakua hawawezi kuongea kutembea na vitu vingine vya kibinadamu kila siku.

Rosemary ambaye pamoja na historia yake kuonyesha amepiga hatua, yeye mwenyewe anasema 'mafanikio bado nayatafuta mpaka sasa na siwezi kusema nimefanikiwa, bado napambana na New York'