Mwimbaji wa Zambia mwenye hit ya Amarulah, Roberto

DStv yakutana na mwimbaji Roberto wa Zambia mwenye hit single ya Amarulah.

Millard Ayo ambaye ni Ripota wa DStv.com upande wa Tanzania alikutana na mwimbaji staa wa hit single ya Amarulah. Mzambia Roberto ambaye kwenye vitu vingi alivyoongea, hivi ni vitano unatakiwa kuvijua.

Patana na wasanii wenye hits kama Diamond, Vanessa Mdee, Ali Kiba na wengine wengi kwenye Mzooka unayoletewa kwenye channel mpya Maisha Magic Bongo (DStv Channel 160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.

 
1. Hakuwa anamaanisha kuimbia kinywaji kwenye wimbo wa Amarulah bali msichana mrembo tu na alijua kabisa lazima itakua hit song.
 
2. Alizaliwa Zambia lakini amekaa sana na kusoma South Africa.
 
3. Kabla ya kutoa 'Amarulah' aliwahi kuja Tanzania zaidi ya miaka miwili iliyopita kwa safari ya kibiashara lakini pia kufanya utafiti ni aina gani ya muziki Watanzania wanaupenda.
 
4. Wasanii ambao amekua akiwafahamu kutoka Tanzania ni Profesa Jay, Vanessa Mdee, Ali Kiba na Diamond Platnumz.
 
5. Pamoja na kwamba kwa sasa ni maarufu na Watanzania wengi wamemjua kutokana na hit single ya 'Amarulah', Roberto kabla ya hapo alitoa album mbili zenye nyimbo nyingine kali lakini 'Amarulah' ndio ikapenyeza kuliko zote.