Staa wa soka Tanzania Mbwana Samatta

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ni miongoni mwa wachezaji wa Tanzania ambao vijana wengi kutoka bongo wanamtazama kama mfano wa kuigwa.
 
Mengi ya soka, usikose kutazama mechi kati ya Tottenham Hotspur na Manchester United siku ya Jumapili 14 May saa 17:30 CAT ndani ya SuperSport.
 
Leo naomba nikusogezee vitu vitano ambavyo inawezekana huvifahamu kuhusu staa huyu Mbwana Samatta ambaye ni moja kati ya wachezaji wanaofanya vizuri kwa kipindi kutoka Afrika  Mashariki.
 
1. Mbwana Samatta anapenda kuvaa viatu vya Nike kiasi kwamba alishawahi kupokea ofa ya udhamini kutoka kwenye kampuni ya Adidas akaikataa kutakoana na mapenzi aliyonayo kwa Nike.
 
2. Anamtazama staa wa timu ya taifa ya Ureno na Club ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kama role model wake.
 
3. Ana uwezo wa kupiga mashuti kwa  kutumia miguu yote kama ilivyo kwa role model wake Cristiano Ronaldo ambaye nae ana uwezo huo ambapo kwa kawaida sio wachezaji wote wanauwezo wa kutumia miguu miwili uwanjani ama  kupiga shuti kwa kutumia miguu yote.
 
4. Alipokuwa anajiunga na timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji alishauriwa na madaktari wa timu hiyo kuwa anapaswa kula vyakula vya kuongeza sukari mwilini kwa sababu alikuwa ana wanga (fat)  nyingi mwilini. 
 
5. Mshahara wa kwanza katika maisha yake ya soka kulipwa ilikuwa shilingi laki tatu (Tsh 300,000) ambayo alikuwa akilipwa na timu ya African Lyon ambayo ilikuwa ikimilikiwa na bilionea wa 16 Afrika Mohamed Dewji.