Director wa video za bongofleva Tanzania Hanscana

Director wa bongofleva Tanzania Hanscana aelezea vitu ambavyo Watanzania hawajui kumhusu

Hanscana ni director Mtanzania ambaye mikono yake imehusika kwenye kutengeneza video za wakali kadhaa wa Bongofleva mpaka sasa akiwemo Vanessa Mdee, G Nako, Jux, Diamond na wengine.

Wasanii hawa waliotengenezewa video na Hanscana unaweza kutana nao kwenye Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Hanscana amekaa kwenye exclusive interview na DStv.com kupitia ripota Millard Ayo na kueleza vitu ambavyo Watanzania wengi hawavijui kuhusu yeye.
 
1. Mara yake ya kwanza kupanda ndege alilipiwa ticket na Diamond Platnumz, ilikua ni siku aliyotoka Zanzibar kufanya video ya Diamond ya Nasema Nawe.
 
2. Ada ambayo msanii anatakiwa kumlipa kutengeneza video na yeye nje ya gharama za video ni shilingi milioni 3.5.
 
3. Haikuwa rahisi kwa mama yake mzazi kumuamini na kumwachia afanye kazi ya kutengeneza video, alikua anamtolea mfano Director Adam Juma kwamba ni tajiri na anaishi vizuri sababu tu ya kufanya video, hiyo ndio ilimfanya mama yake kumruhusu Hanscana kuwa director.
 
4. Kuna baadhi ya Ma-director wenzake wamemkasirikia na wakati mwingine hawaongei nae kwa sababu akihojiwa kuhusu nani mkali kwenye media huwa hawataji.
 
5. Video yake iliyomfungulia milango na kuanza kuitwa na mastaa kuwafanyia video ni ambayo aliifanya na Navy Kenzo, baada ya hapo akapigiwa simu na Vanessa Mdee kufanya video ya siri, kilichofata ni umaarufu na kazi nyingi mfululizo.