Chris Brown at a past performance

Tunafahamu kuwa mkali wa Hip Hop and RnB kutoka nchini Marekani Chris Brown aliperform usiku wa Mombasa Rocks Music Festival wikendi huko Mombasa Kenya katika uwanja wa Mombasa Golf Club akiambatanza na wasanii wengine kama Alikiba na Vanessa Mdee kutoka Tanzania, Wizkid wa Nigeria, Navio wa Uganda na wengineo wengi.

Patana na Chris Brown tena kenye Mziki Fresh, Jumatatu hadi Ijumaa saa 18:00 kwenye TRACE Mziki (323).

DStv.com inakusogezea mambo matano ambayo yalikuwepo kwenye show ya mkali huyu ambavyo vilikuwa vya kipekee na havijawahi kutokea kwenye show ya msanii mgeni Afrika Mashariki.
 
1.Chris Brown ameletwa na private jet pamoja na crew yake all the way kutoka Marekani mpaka nchini Kenya na sio ndege ya abiria kama ilivyokuwa kwa wasanii wengine wanavyoletwaga.
 
2.Chris Brown amelipwa kiasi cha shilingi Milion 90 za Kenya ambazo ni zaidi ya Billion moja na million tisa za kitanzania na ilikuwa show ya muda wa dakika 90 tu.
 
3.Msanii huyu alilazwa chumba chenye hadhi ya Rais kwenye Hotel ya English Point Marina, Mombasa yenye hadhi ya nyota tano chenye thamani ya laki moja na elfu hamsini ya Kenya ambayo ni sawa na zaidi ya million tatu na laki mbili za kitanzania yani Million 3,230,700 Tshs.
 
4.Msafara wake ulikuwa na hadhi kubwa wenye magari 6 na helicopter moja juu ya ulinzi na usalama ikisindikiza pamoja  gari ya polisi iliyokuwa mbele kuongoza msafara huo.
 
5.Pia Chris aliperfom show hiyo ndani ya dakika 90 ambazo zilipangiliwa na ikiwa kama sababu ya wasanii wengine kuwa na perfomance fupi ili aperfom na kurudi kuanza safari yake kurudi Marekani baada tu ya kutoka kwenye show hiyo ikiwa na maana kuwa hakulala Mombasa usiku huo.