Bilionea Hellen Dausen

Hellen Dausen ni mrembo wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 29 ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa vijana 30 wa Afrika ambao ni mabilionea wa siku chache zijazo.

Jarida la Forbes ambalo ni maarufu kwa kutoa takwimu na ripoti mbalimbali za watu na pesa zao, watu na harakati zao lilimtaja Hellen na Mtanzania mwingine mmoja aitwae Edwin kuwa ndio watanzania pekee kwenye list hiyo ya Mabilionea 30 ambao watakua mabilionea baadae na kuajiri maelfu ya watu.
 
Mbali na Watanzania hawa mabilionea, pia kutana na mastaa wengine kutoka Tanzania kwenye Inside Bongowood, Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo
 
Hellen ni bilionea wa siku chache zijazo lakini pia ni mtu anaependa burudani japokuwa ana zaidi ya mwaka mmoja hajawahi kwenda night club.
 
1. Anasema toka ameanza kuwa mjasiriamali amekua na mawazo ya tofauti na hata msukumo wa kustarehe sana kama kutoka kwenda night club umepungua kwa kiasi kikubwa, kila siku anawaza anapigaje hatua za keshokutwa.
 
2. Miongoni mwa wasanii ambao anasikiliza sana nyimbo zao ni pamoja na Vanessa Mdee kama Nobody But Me, Niroge na Nitajuta ya Yamoto Band.
 
3. Starehe yake kubwa ni kwenda ufukweni ambapo anasema, "Napenda sana kwenda kulala beach, nitalala hata masaa matatu na inanisaidia kupata mawazo mapya au kuyajenga niliyonayo."
 
4. Series ambayo amewahi kuitazama na hatoisahau ni Prison Break, ni series ambayo hata akiambiwa arudie kuitazama hatokataa japo ametazama series nyingi, hiyo ni namba moja kwake.
 
5. Channel ambazo huwa anazitazama sana kwenye King'amuzi cha DStv ni pamoja na E! na MTV Base.