Msanii wa Tanzania Belle 9

DStv yakutana na msanii wa bongofleva Belle 9

Belle 9 ni mwimbaji staa wa bongofleva na jina lake limekua miongoni mwa majina mazito ya bongofleva kwa zaidi ya miaka mitano sasa kutoka na hits alizodondosha ndio maana nikaona leo nikusogezee haya mambo matano yanayomuhusu.

Patana na Belle 9 na muziki yake kwenye Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo (160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.

 
1. Alishawahi kuwa kundi moja na mwimbaji Dayna ambaye anafanya muziki wa bongofleva pia, waliwahi kundi moja la muziki enzi hizo wanaanza mkoani Morogoro.
 
2. Pamoja na kwamba wazazi wake walikua wakali, Belle 9 aliwahi kuulizwa anataka kufanya muziki au shule? Na aliwajibu wazazi wake kwamba anataka kufanya muziki na safari ndio ikaanzia hapo.
 
3. Mpaka sasa hivi Belle 9 hatumii kilevi chochote kwenye maisha yake na hajawahi kuona umuhimu wa kutumia kilevi kabla ya kupanda kwa stage, siku zote amekua live bila kilevi na ameshazoea na anafanya bila woga.
 
4. Ameshawahi kufanya biashara kadhaa kabla ya kutusua kwenye muziki, Belle 9 alishawahi kufanya kazi kwenye kiwanda cha Tumbaku Morogoro enzi hizo baada ya kushindwa kuendelea na shule.
 
5. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 Belle 9 alipatwa na kiu ya kupata pesa ili alipie studio hivyo alilazimika kuuza bidhaa ndogondogo kwenye stand ya mabasi Morogoro ikiwemo kuuza Mayai na Juice.
 
Kurekodi muziki ya wasanii wa bongofleva kama Belle 9 kwenye Maisha Magic Bongo, jaza fomu hii upate Explora yako itakayokuwezesha kurekodi na pia kuchezesha tena muziki hii: