Ernest Napoleon in Going Bongo

Mtanzania Ernest Napoleon ametengeneza movie inayosifiwa kote, jua mengi kuhusu movie hii.

Going Bongo ni movie ya Mtanzania Ernest Napoleon ambaye alizaliwa Urusi na akaishi kwenye nchi kama Tanzania na Marekani ambako ndiko alipata ujuzi wa uigizaji na utengenezaji wa filamu.

Kujua mengi kuhusu Bongowood, tazama Inside Bongowood kila Alhamisi saa 16:30 kwenye Maisha Magic East.

Kwenye hii post nimekusogezea mambo matano kuhusu yeye na movie yake ya Going Bongo.

1. Ni movie ambayo ilitengenezwa Marekani na Tanzania na iligharimu zaidi ya milioni 500 za Tanzania.

2. Tofauti na movie nyingine za Watanzania ambazo huchukua muda mfupi kukamilika, movie hii imetengenezwa kwa maika miwili na nusu na ilichukua muda mrefu pia kutokana na pesa.

3. Miongoni mwa nchi za Ulaya zilizoongoza kwa kuinunua hii movie ni Ujerumani na Marekani.

4. Baada ya kuionyesha kwa mara ya kwanza Uingereza, Ernest ametumiwa maombi ya wamiliki wa kumbi za cinema ambao wanataka kuanza kuionyesha kwenye majumba ya Cinema Uingereza.

5. Movie hii ya Going Bongo imeshinda tuzo kwenye tamasha la ZIFF 2015 huko Zanzibar kama movie bora ya Afrika Mashariki.

 Unaweza kutazama trailer yake kwa kufuata hii link.