Idris Sultan

List ya mastaa wa Tanzania waliotumia majina yao (Brand) kufanya biashara inaongezeka

Mastaa mbali mbali duniani wenye majina makubwa wamekuwa wakitengeneza pesa nje ya tasnia zao kwa kutengeneza bidhaa ama kuingia ubia na makampuni mbalimbali ili majina yao yatumike kwenye bidhaa kama nguo, manukato, urembo, viatu na hata vyakula.

Hapa Tanzania tumeona mastaa mbalimbali wakiyatumia majina yao katika kutengeneza pesa zaidi. Mifano ni kama   Jokate Mwegelo ambaye wiki chache zilizopita jarida la Forbes lilimtaja katika orodha ya 30 under 30, wajasiriamali wakutazamiwa zaidi 2017 akiwa na brand yake ya  Kidoti inayotengeneza bidhaa za nywele, sandles pamoja na mabegi. 

Mwingine ni Diamond Platnumz aliyetambulisha marashi yake ya Chibu Perfume na hivi karibuni ametuletea bidhaa ya karanga yenye jina lake.

Wema Sepetu ambaye alikuja na lipstick zenye jina lake, Kundi la Weusi, Jux pamoja na Vanessa Mdee ambao wanatengeneza pesa kupitia majina yao.

Mengi ya bongo, tazama Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160).

Mtu mwingine ambaye tunategema kuona bidhaa yake ni Idris Sultan ambaye ametangaza ujio wa bidhaa yenye jina lake, huku wengi wakihisi inaweza kuwa perfume ama mafuta ya kujipaka  kutokana na jina ambalo Idris mwenyewe ameiita bidhaa hiyo #SultanByForMen ambayo amesema tutegee kuipata mwezi August mwaka huu.

Pia soma mengi kuhusu Wema Sepetu na filamu yake mpya.