Heshima ya Ndoa

Hii Oktoba, Maisha Magic Bongo inanendelea kuangazia filamu za mapenzi yaani romance. Mara kwa mara ni vyema kuchukua muda kufurahia na washikaji wetu. Wakati mwingine, tunapata shida katika mahusiano lakini hatimaye lazima tupate kwendelea. Tuangalie jinsi unaweza jua kama mpenzi wako ameanza kukuchezea moyo yani playing games zisizotakikana!

1. Pesa kabla Mapenzi

Pesa ni sabuni ya roho. Lakinia pia ni rahisi sana kukosanishwa na pesa kati ya marafiki au wapenzi. Ukianza uhusiano wowote jitahadharishe na kuchanganya burudani na fedha. Wapenzi ambao wanapenda kutumia benki na akaunti moja, hii si jambo la busara. Wakati wowote mmoja wenu anaweza taka kununua kitu ama kwenda likizo. Je, unaweza fikiria vile ambavyo maisha ingekuwa kama mpenzi wako angekua hana pesa ama kazi?

Tazama Heshima ya Ndoa, Jumamosi 24 October saa 14:00.

 

2. Maisha ya anasa

Tunapenda kufuatilia maisha ya wale celebrities tunaowatazama kwenye televisheni ama ambao tunawasikiza kwenye radio. Ni muhimu kutambua ya kwamba maisha zao si zetu ili nasi pia tuishi virahisi bila shinikizo. Kuelewa vyema hii hali, tazama filamu ya drama romance kuhusu Papiki and Lizzy, wapenzi ambao wanakosana kwa sababu ya uchoyo wa mmjoa wao anayetaka kuishi maisha ya kifahari.

Tazama Safari Yangu siku ya Jumanne 27 Oct saa 17:00.

 

3. Wakosanao ndio wapendanao

Uhusiano yoyote ile ni lazima kupata shida mara kwa mara. Wakati mwingine ni mpenzi wako kutokupenda ulivyo ama kutotaka uhusiano kama ndoa  sababu ya shida za nje kama kazi. Hii Oktoba, tazama filamu kuhusu kupoteza mapenzi, na kupata mapenzi. Kumbuka maisha kitenesi leo mimi kesho wewe.

Tazama Tensus siku ya Jumatano 28 Oct saa 18:30 na Amar Akbar Anthony siku ya Ijumaa 30 October saa 16:00.