shilole kwenye interview na Millard

Sasa kinachoendelea sasa hivi ni stori za kuachana kwa Nuh Mziwanda na Shilole ambao wote ni wasanii wa bongofleva. Shilole hakuwa anataka kuongelea hii ishu kabisa na hata majibu yake yamekua ya mkato.

Ukiwa unafatilia stori za mastaa wa bongo na maisha yao basi na hii utataka kujua ilikuaje? kinachoendelea na imeishia vipi?

Zaidi ya miezi miwili iliyopita Shilole alihojiwa na Millard Ayo na kukiri yuko tayari kuolewa na Nuh, hata wakati huo Nuh angeamua kumuoa angekubali tu sababu wanapendana na alifuta kauli yake kwamba hatoolewa tena baada ya kuachana na mume dereva wa lori aliyemtesa.

Sasa kinachoendelea sasa hivi ni stori za kuachana kwa Nuh Mziwanda na Shilole ambao wote ni wasanii wa bongofleva. Shilole hakuwa anataka kuongelea hii ishu kabisa na hata majibu yake yamekua ya mkato.

Millard: Sababu za kuchana na Nuh ni zipi?

Shilole: We jua sipo nae tu.... siwezi kumzungumzia tena na sitaki, sitaki tu

Millard: Ni kweli umeifuta tatoo ya Nuh uliyokua umejichora?

Shilole: nimeifuta, na kuifuta mwilini inauma lakini ndio hivyo, maamuzi niliyafanya baada ya kuchefukwa.

Millard: Utakubali Mwanaume mwingine kuja kwenye maisha yako baada ya hii?

Shilole: Mi ni binadamu na ni Mwanamke, napendwa na ninatongozwa kila siku... sijajua ila kupenda kwa sasa hivi bado.

Kila mtu na starehe zake kweli!  Kwa masuala ya ndoa na kadhalika Bi Mariam Wamigambo anatuletea mawaidha ya kinyumbani, ubinafsi, tabia njema na desturi za wanawake katika kipindi kipya Mchichimko wa Pwani! Ungana nasi basi kila Jumatano saa 18:00 CAT hapa Maisha Magic Bongo!