Mrembo Jokate kutokea Tanzania ambae ametajwa mara kadhaa kusemekana kuwa kwenye mahusiano na Alikiba wa Bongoflevani takribani tangu miaka miwili iliyopita .

Wawili hao walishahojiwa mara kadhaa lakini hakuna aliewahi kukiri kuwa wako mapenzini, kama nimfatiliaji mzuri wa mitandao ya kijamii utakuwa unafahamu kuwa 29 Novemba ilikuwa siku ya kuzaliwa ya msanii Alikiba ambapo ametimiza miaka 30.

Burudika na nyimbo mpya za King Kiba kwenye show ya Bongo 10 kila Ijumaa saa 20:00 ndani ya Trace Mziki (323).

Jokate aliandika maneno kwenye instagram yake ambayo yalikuwa ya lugha ya kigeni, lugha ya kifaransa ambayo tafsiri ya maneno hayo kwa kiswahili aliyomuandikia kama salamu za birthday yanayodhiirisha kuwa nae kimahusiano ya mapenzi.

Mrembo huyu aliandika hivi Baby happy birthday I love you so much, it hurts. I want nothing but the best for you from the bottom of my heart, the rest I leave to God for what happens to know that Jojo doesn’t worry and that am happy to have you as my friend. Be blessed”.

Bado Alikiba hakuhakiki juu ya hili lakini hayo ndo mambo yanavyonekana kwa wawili hawa.

 

Related