Mwigizaji Aunty Ezekiel

Aunty Ezekiel apeana mawaidha kwa wasichana na wanawake kuhusu uja uzito.

Wakati huu mwigizaji Aunty Ezekiel akikaribia kujifungua mtoto anaetajwa kuwa wa dancer wa Diamond Platnumz, Moses Iyobo kuna machache anayoongea na wanawake au wasichana.

Aunty amesema kwamba kwa yeyote anapata ujauzito na akautoa ana hatari ya kukosa au kupata taabu ya kupata mtoto, hivyo tabia ya kutoa ujauzito iachwe.

Ungana na waigizaji wengine kwenye filamu ya God's Kingdom Jumapili saa 19:00 CAT kwenye Maisha Magic Swahili. Pia, burudika na filamu unazozipenda kila wakati kwa kudownload app ya DStv Now kwa simu yako ya iOS na Android.

Aunty aliwahi kupata tatizo lakini sio kwa sababu ya kutoa ujauzito bali kupigwa na boyfriend wake aliyekua akiishi naye, ujauzito aliokua nao ulifikia miezi saba lakini baada ya kupigwa ukaharibika.

Anasema boyfriend wake huyo alikua kama ni mtu mwenye jini hivyo alikua akikupiga hachagui pa kukupiga na alimpiga sana tumboni mpaka ujauzito ukaharibika.

Kuhusu ujauzito wa sasa Aunty amesema anatarajia mtoto wa kike lakini bado mpaka sasa hajajua jina lipi watampatia kati ya waliyoyapata.