Mkubwa Fela kutoka Tanzania

Leo tunae Said Fela mkimfahamu kama Mkubwa Fela au Mkubwa na anaeimiliki Yamoto Band lakini pia ni mananger wa wasanii kama Diamond Platnumz,Chegge Chigunda na Temba.

Ngoma za Diamond na pia Yamoto Band inakujia kupitia Mziki Fresh, Jumatatu hadi Ijumaa saa 20:00 kwenye channel mpya ya TRACE Mziki (323).
 
Katika interview hii ameongelea mengi moja wapo atoa majibu juu ya maneno yanayosemwa kuwa anawatumia wasanii walioko chini yake kwa maslahi yake binafsi.
 
Said Fela aliyaongea haya, "Kwanza nilikuwa na prove wrong watu kuwa Fela anafanya mziki kwa sababu ya faida, Mimi niltaaka watu waelewe kwamba natengenza reli watu watengenezee maisha yao."
  
Aliendelea, "Kwamba nawasaidia wasanii kwasababu mimi nimesaidiwa toka nilivyokuwa South Afrika mpaka nimepata mafanikio, nimerudi nyumbani nikaone pia nifanye hichi kitu."
 
Said Fela alimalizia, "Nikaanza na TMK wengine wakajiona wao ndo wana maana lakini mpaka leo nmenyanyua wasanii wengi najivunia nimefanya kitu kwa Tanzania hata nikifa kesho asubuhi kuna watu ambao watakuja kunikumbuka tu."