Sallam kutoka Tanzania

DStv.com inahakikisha hupitwi na chochote kinachotrend sasa hivi mtu wangu, leo kwenye hii post tunamsogeza mananger wa Diamond Platnumz, Sallam K ambae alikuwa na tuhumu kutoka kwa Alikiba kudai kumzimia mic wakati akiperfom kwenye stage ya Mombasa Rocks Music Festivals.

 
Baada ya kupatikana kwa Sallam K, manager huyu wa Diamond Platnumz alitoa majibu ndani ya sentensi nane kuhusu tuhuma hizo kama iifuatavyo hapo chini
 
1. Alikiba kama amekosea yeye anatakiwa kuomba radhi mashabiki wake na promota, pia aombe Mungu next time kila kitu kiende vizuri.
 
2. Wakati Alikiba anatumbuiza sikuwepo kabisa katika stage hata karibu sikuwepo, nilikuepo katika stage wakati Chris Brown na Wizkid wakitumbuiza.
 
 
3. Alikiba kauliza kwa nini nilikuwepo show ya Mombasa, kitu anatakiwa kujua mimi sio meneja wa Diamond pekee, nina mengine nafanya.
 
4. Alikiba kama ana chuki na Diamond aangalie jinsi gani anaweza kuzimaliza kuliko kila kitu kusema meneja wa Diamond au Diamond.
 
5. Sikuwepo peke yangu kwenye show ya Mombasa, Sauti Sol na meneja wao, Bebe Cool pia alikuwepo lakini hawakualikwa kutumbuiza.
 
6. Alikiba alichelewa kupanda kwenye stage kwa lisaa lizima tofauti na alivyopangiwa, timu ya Chris Brown ndio iliyomtoa kwenye stage.
 
7. Nataka kuweka wazi Alikiba hata akiniona back stage asiwe na wasiwasi sababu tutakutana MAMAs huko South Africa, asiogope.
 
 

8. Alichosema Alikiba sijataka kubishana nae nimechukulia changamoto, nimemsamehe kwa roho safi na sina kinyongo nae.

Burudika na Alikiba na pia Diamond kwenye show ya Mzooka Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.