Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz

Leo tuko nae staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz mmiliki wa hit song iliyopata mapokezi makubwa sana ya Salome.

Burudika na nyimbo za Diamond kama Salome kwenye kipindi cha mziki cha Mzooka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Well najua kuna wadau wangu ni wapenzi wa kufuatilia maisha ya wasanii wao hapa bongo, siku chache Naseeb Abdul mkimfahamu kama Diamond Platnumz alipost picha kwenye instagram ya nyumba ya South Afrika na kwa madai kuwa ni ya kwake ameinunua.
 
Nyumba hii iliibua maswali mengi kwa mashabiki na utata ukatokea kuwa nyumba sio ya kwake, na leo kwenye hii post unapata majibu kamili kutoka kwake mwenyewe Diamond.
 
"South Afrika nyumba zinakuwa kwenye site online utakayoipenda unapress oder, kuna 10 percent unatoa kwanza kuonesha kama uko serious then unamalizia malipo ili wakufanyie transfer kwenda kwenye majina yako hapa nimetoka bank kufanya malipo ya transfer ili wapeleke kwenye majina yangu," Diamond alisema.
 
Diamond alimalizia, "Hayo ni maneno tu watu wanapost kwenye media ambayo hayana ukweli, nyumba ni yakwangu na kwa pesa ya kitanzania inagharama kwenye million 400 mpaka 600 hivi."