Mtanzania Majani

P-funk Majani ni mmoja kati ya watayarishaji (producers) nguli wa muziki Tanzania ambao wana heshima kubwa kwenye muziki wa bongofleva akiwa kati ya waanzilishii wa mwanzo kwenye utayarishaji wa hits bongo.

Majani alikaa kimya kwenye game kwa muda mpaka mwaka huu ambapo ameamua kurudi kwenye game upya yaani kutayarisha midundo tena huku akitambulisha kundi jipya chini ya label yake ya BongoRecords.

Majani anasema mziki bongo sasa hivi umebadilika sana sio kama zamani ambapo hip hop ilikuwa haiuzi sana huku akisema kipindi hiki hip hop imekuwa kama miziki mingine inayofanyika kwenye bongo fleva.

Burudika na wasanii wa hip hop kutoka bongo kama Darassa, AY na wengine kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160).

Mbali na Diamond, P-Funk alimtaja rapper Darassa kuwa kati ya watu waliompa mzuka wa kurudi tena kwenye game.

Majani alisema, "Yule dogo Darassa anaipeleka hip hop ya Tanzania kimataifa, wakina Weusi pia yani vijana wameamka mpaka nafurahi kurudi kwenye game najua tutatengeneza kazi nyingi sana."

Uliyaskia ya Lavalava, msanii mpya kwenye WCB?