South African duo Mafikizolo

DStv yakutana na kundi la South Africa Mafikizolo

Ni kundi la muziki kutoka Afrika Kusini ambalo limefanikiwa kupata mashabiki wengi upande wa Afrika Mashariki pia na hata hit single yao ya Khona kuchezwa sana kwenye maharusi mwaka 2014.

Tunafahamu kuhusu kolabo yao ambayo waliirekodi mwaka jana na msanii wa Tanzania nchini South Africa kwenye studio ambako ndio kulirekodiwa hit single ya Khona.
 
Burudika na hit single hii ya Khona na mengine mengi kwenye Base Lines Jumamosi saa 17:00 kwenye MTV Base.
 
Walipofika Tanzania na kukutana na reporter wa dstv.com Millard Ayo, Mafikizolo waliulizwa kuhusu hiyo kolabo ambayo haikutoka mpaka sasa na wakajibu bado wako busy na kolabo na Wasanii wa Nigeria, Guinea, Kenya na msanii kutoka Tanzania ambaye hawakumtaja.
 
Mafikizolo hawakutaka kuweka wazi ni msanii gani na kama ni wa kike au wa kiume lakini wanasema wamefanya nae wimbo mkali sana na ni wimbo wa kudance, wanaamini utabamba sana.
 
Kauli ya Mafikizolo inaleta maswali mengi kama ni Diamond ama la manake wamegoma kabisa kumtaja sasa hivi lakini wakati wanarekodi South Africa walipost na picha, haijulikani kama atakua ni msanii mwingine tofauti na Diamond

Related