Msanii wa Tanzania Darassa

Kwa mashabiki wa msanii kutoka bongoflevani Darassa, tunae kwa ajili ya hit song yake Too Much ambayo kiukwel imepata mapokezi mazuri kwenye game.

Kutana na msanii huyu Darassa na wimbo wake wa Too Much kwenye kipindi cha mziki cha Mzooka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo

Kwenye exclusive na DStv, Darassa amefunguka juu ya mafanikio alioyapata kutokana na ngoma hii baada ya ukimya wa mda mrefu.
 
Msanii huyu ameyazungumza haya, "Unajua toka nimeingia kwenye game lengo langu limekuwa kujikuza kila siku kuwa mtu mkubwa you know."
 
Aliendelea, "Nafanya kazi kila siku na project ya Too Much kuwa hit kubwa ambavyo imekuwa. Tayari imeshakusanya watu wengi na imefanya watu wote kuwa attention kwamba nikitoa nyimbo wanajua Darassa ametoa nyimbo."
 
Alimalizia, "Too Much imehit haraka na kilichotokea imenifanya nimekuwa mtu mkubwa ambapo kila siku ilikuwa ndio ndoto yangu na ndio kitu ambacho natakiwa kufanya na imeniwezesha kufanya vitu vingine'.