Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

DStv yakutana na dadake Dr. Magufuli ambaye adakua machache kuhusu rais huyu mpya

Ripota wako wa dstv.com Millard Ayo anakuletea machache kutoka kwenye familia ya Dr. Magufuli yatayotupa nafasi ya kumjua Rais huyu mpya wa Tanzania kwa upande wa pili.

Pia unaweza kujua mengi kuhusu mastaa wa Tanzania na maisha yao kwa kuitazama kipindi cha majadiliana Mkasi kila Jumapili saa 16:00 EAT kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Dada yake wa pili anayefuatwa na Dr. Magufuli ndio anayasema haya ambayo inawezekana tulikua hatuyajui kumhusu Rais huyu mpya.
 
1. Dada amesema Dr. Magufuli akiwa mdogo alikua anapenda kusoma, kucheza na kutengeneza tuvituvitu na alikua mchapakazi.
 
2. Kingine ni kwamba Dr. Magufuli alivyokua mdogo alikua mtiifu sana na anafanya kazi za nyumbani bila ubishi ikiwemo kuosha vyombo kwa zamu.
 
'Hata mkipangiwa kwenda shambani Magufuli hakuwa anakataa chochote, alikua hana ubishi kushika jembe, kilimo tumelima na alikua anajituma sana' - Dada.
 
3. Kingine ambacho inawezekana ulikua hukifahamu ni kwamba Dr. Magufuli aliwahi kuwa mwalimu wa sekondari kufundisha Sengerema Mwanza.
 
4. Kwa kumalizia, Dada huyu wa pili kuzaliwa kwenye familia ya kina Magufuli amesema anaamini yale Dr. Magufuli aliyoyasema kwenye kampeni atayafanyia kazi kikwelikweli sababu ndio yamempa nguvu ya ushindi.