Msanii Ali Kiba

DStv yakutana na King Kiba kujua mengi kumhusu na muziki yake

Ripota wetu Millard Ayo anatusogezea stori zote kutoka upande wa Tanzania kupitia hapa DStv.com kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo na stori nyingine kwenye headlines.

Leo kuna exclusive kali na mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba, ambaye amekaa na kuyajibu maswahi haya machache.

1. Kwanini Alikiba hauhudhurii kwenye tuzo unazowania?

Jibu alilolitoa ni hili: “Ninapokua naona kuna umuhimu wa kwenda nitakwenda, napendaga kuhudhuria lakini napenda mimi kufanya kitu ambacho nahisi au natamani kufanya. Nimegundua kwamba mimi ni mwanamuziki ambaye siwazii sana tuzo, muziki wangu unathamani zaidi ya tuzo, mimi mwenyewe ni mkubwa zaidi ya tuzo hivyo itakapokuwa na ulazima nitakwenda lakini kama hakuna ulazima nitaendelea kufanya biashara zangu.”

2. Kuhusu kutoa single mpya. Utatoa lini kaka braza?

Alikiba amesema sasa hivi sauti yake itasikika kwenye kolabo mpya aliyofanya na mwimbaji Christian Bella inaitwa Nagharamia ambayo ameitaja ni kama movie na iwapo kuna mtu anaweza kujitokeza na kutoa milioni 700 wanaweza kumuuzia hiyo stori.

3. Nini kipya katika camp ya Alikiba?

Alikiba ameahidi kuja na kitu tofauti yani mguso tofauti kwenye muziki wake baada ya kurudi kutoka Marekani, anasema itakua ni suprise hivyo hawezi kusema kama itakua ni kolabo au ni kitu gani ila mashabiki wajiandae tu kwa kupokea kitu kikali kutoka kwake.

4. Kati nyimbo za bongo ambazo ziko rotation saa hii gani unaipenda sana?

Miongoni mwa nyimbo mpya za bongofleva anazozisikiliza sana kwa sasa ni pamoja na mpya ya Samir na Nivumilie ya Baraka da Prince na Ruby.

Haya basi kwa mziki wa kukata na shoka toka Afrika Mashariki, tazama Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye channeli mpya iliyozinduliwa ya Maisha Magic Bongo.

Pamoja na muziki, Maisha Magic Bongo pia inakuletea filamu kali pamoja na vipidindi kem kem vya kuburudisha!