Wema Sepetu

Kwenye exclusive interview ya mbeleni na DStv.com mwimbaji wa bongofleva Linah alisema hana beef na mwigizaji Wema Sepetu japo hakupendezwa na kitendo cha Wema kuonekana na boyfriend wa Linah wakati hawakuwa wameachana.

Kwenye magazeti na mitandao ya habari za mastaa Tanzania kuliandikwa kuhusu Linah kutokuelewana na Wema ambapo kwenye hii interview ya dstv.com, Linah aliweka wazi kwamba hakuwa ameachana na boyfriend wake huyo bali walikuwa wamenuniana tu kitu ambacho ni kawaida kwenye mapenzi ya kila mtu.
 
Ukitaka kujua mengi kuhusu wasanii wakubwa Tanzania na maisha yao, usikose kuitazama kipindi cha majadiliana Mkasi kila Jumapili saa 16:00 EAT kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Sasa wanaofatilia walijiuliza maswali baada ya Linah kuonekana kwenye birthday party ya Wema Sepetu  2 Novemba  ambapo baada ya hapo tumempata Linah kuelezea Watanzania wanachotakiwa kukielewa.
 
"Party ya Wema Sepetu ilikua nzuri, nilipatiwa kadi ya mwaliko kama wageni wengine wote walivyoalikwa na kiukweli nilijisikia faraja sana kualikwa, mimi na Wema hatujawahi kugombana."
 
 
Linah kaendelea kusema, "Kupishana kidogo ni vitu vya kawaida kwenye maisha ya binadamu, Watanzania waelewe kwamba hivyo ni vya kawaida, kuna ups and downs, alinialika kwenye birthday yake nikaenda kushow love, na huwa tunachat na nipo hata kwenye group yake ya Whatsapp hata leo tumechat, tumeachana na yaliyopita."
 
Kweli yaliyopita si ndwele.Tuyagange yajayo. Points kwako Lina!