Msanii wa bongofleva Linah

Msanii wa bongofleva Linah asafiri nje ya Tanzania kwa project ya 2015.

Ujazo wa jina la mwimbaji wa bongofleva Linah uliongezeka kwa kiasi kikubwa baada ya kuachia hit single ya Ole Themba aliyoifanya nje ya Tanzania, yaani Afrika Kusini.

Kuburudika na muziki zingine, ungana na DJ Tass kwenye Wakilisha, Jumatatu hadi Ijumaa, saa 17:00 kwenye Maisha Magic Swahili.

Kingine Linah alichokitoa kupitia dstv.com ni kwamba anasafiri kuelekea nje ya Tanzania kwa ajili ya kazi yake nyingine kutoka kwenye project ya mwaka 2015.

Linah ambaye alifanya video ya Ole Themba na director God Father wa South Africa, amesema kuna kazi nyingine iko mikononi mwa mkali anaeheshimika Afrika kwenye ishu ya burudani na ndio itakayofata kwa kutolewa.

Baada ya hapo najua unaweza kuwa na maswali mengi, Ni video mpya inafuata? Au kolabo na mkali mwingine wa Afrika? Majibu yote haya Linah ameahidi kuyatoa wiki ijayo hapahapa kwenye dstv.com.

Linah ameondoka kwenye uwanja wa ndege Dar es Salaam kimyakimya bila picha yoyote lakini akaruhusu watu wake waambiwe tu kwamba kaondoka Tanzania, alichokifata atakitaja soon.

Wakati unasubiria hizo good news, sasa hivi endelea kuburudika na single yake mpya ft. Christian Bella - Hello ambayo inachezwa pia kwenye Wakilisha, Jumatatu hadi Ijumaa, saa 17:00 kwenye Maisha Magic Swahili.