Msanii Linah Sanga

Kutana na mwanadada msanii kutoka Tanzania Linah Sanga ambaye pia amewahi kuigiza katika bongo movies hapo awali. Linah kwa sasa hivi anatambaa na hit single yake mpya ya Raha Jipe Mwenyewe.

Ungana naye kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo saa 16:00 Jumatatu hadi Ijumaa.

Tulikutana na msanii huyu alipokuwa kwenye media tour yake Nairobi, Kenya na akaongelea muziki wake, haswa matarajio ya mwaka mpya wa 2017. Linah ambaye amekumbwa na utata kuwa ana mahusiano na Idris Sultan alielezea wazi kuwa hamna kitu kati yake na mshindi huyu wa Big Brother ila tu ni marafiki tangu zamani. Alichukua nafasi hii kumtaja Director Ghost kama mpenzi wake.

Pia ulisikia ya Ben Pol na kujisifu kuwa msanii wa kwanza kuleta muziki wa RnB uwanjani?

Kasema haya:

 

 

Mbali na haya, Linah ana maoni yapi kumhusu Wema Sepetu?