Bongofleva artist MB Dogg

MB Dogg aelezea DStv ni kwa nini akawa kimya kimuziki, na vile anavyopanga kurudi kwenye bongo

Kama unazikubali kazi zake inawezekana ulimfuatilia lakini hapo katikati akatoea kwenye masikio yako sababu hujasikia single yoyote mpya kutoka kwake.

Msanii MB Dogg kakutana na dstv.com kwenye exclusive interview na kueleza kwamba ukimya wake ulitokana na yeye kuhamia Ujerumani na kuishi kwa miaka miwili lakini pia amekua akijipanga kwa ajili ya kurudi bongoflevani.

Kuburudishwa na wasanii wengine kutoka bongoflevani, usikose kutazama performance ya Diamond kwenye MTV Africa Music Awards 2015 saa 21:00 CAT, Jumamosi 18 July kwenye MTV Base.

MB Dogg ambaye alikua chini ya Tiptop Connection miaka kadhaa iliyopita, amesema kwa sasa yuko chini ya kampuni nyingine inayosimamia kazi zake.

Kama ulikua hujui, MB Dogg pia ni mchoraji mzuri wa ramani za nyumba na ameifanya hiyo kazi huku akithibitisha kwamba ni muda mrefu amekua akiifanya kazi na Dar es Salaam kuna nyumba kibao kazichora yeye.