Msanii Fred Wayne

Msanii Fred Wayne aelezea kwa nini alibadilisha dini kutoka Mkristo na kuwa Muislamu

Imekua ni jambo la kawaida kusikia mtu kabadilisha dini kwenye mazingira tunayoishi labda sababu anatakiwa kuoa au kuolewa na mtu wa dini nyingine.

Kwenye exclusive ya leo on DStv.com msanii wa kundi la Makomando bongoflevani Tanzania Fred Wayne amekaa na kueleza ukweli kuhusu kubadili kwake dini.

Exclusive zingine kuhusu mastaa wengine wa Tanzania zipate kwenye Mboni Show, Jumamosi saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Ukweli ni huu, “Sijabadilisha dini kutoka Mkristo kuenda Muislamu sababu na mwanamke, wengi walidhani nimefanya hivyo sababu ya mwanamke, ukweli ni kwamba niliamua tu mwenyewe.”

“Nimekua nikiishi na bibi yangu, na yeye alibadili dini tu so hiyo ni moja ya vitu vilivyonishawishi mimi kubadili baada ya kuanza maisha ya kujitegemea, nikakaa nikapima mwenyewe nikaona kuwa Muislamu itanisaidia, lakini hii haimaanishi kuidharau dini ya Kikristo, kila mtu huwa anachagua moja.”

Fred kwa sasa analo jina jipya pia baada ya kubadili dini.... anaitwa Feisal.