Waigizaji wa Mahusiano

Kutana na Rachel Kuyunga na Barton Mwemba waigizaji wa Mahusiano, tamthilia kwenye CloudsTV

Mwanzoni wakati tunaanza kuigiza baadhi ya wenzetu tuliosoma pamoja waliona kama tumekosea, wanauliza yani kusoma kote mnaishia kwenda kuigiza? Ila sasa hivi maisha yetu yamebadilika na wengine bado hawajapata kazi.

Hayo ni maneno ya waigizaji hawa maarufu wa tamthilia ya Mahusiano ambayo inaonyeshwa kupitia CloudsTV (294) na imekua ikihusu sanasana ishu za uhusiano wa kimapenzi.
 
Picha kubwa wanayoitoa hawa waigizaji Rachel Kuyunga na Barton Mwemba ( Mwijaku) ni kwamba hawakuona kama usomi wao wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ni kikwazo cha wao kuigiza. Na pia Mungu amewasaidia mpaka leo wanayaendesha maisha yao vizuri kutokana na pesa ya kuigiza tu kwenye tamthilia lakini wengi waliomaliza nao chuo hawajapata kazi mpaka leo.
 
Rachel anasema: "Maisha ni magumu sana sasa hivi, kuna watu wasomi na bado wako mtaani maana hakuna kazi, mimi nakomaa hapa hapa kwenye kuigiza na naamini siku moja nitafika mbali."
 
Kikubwa kinachofanyika sasa hivi ni kuifanyia tafsiri ili iweze kukaa kwenye lugha ambayo inaeleweka na Wanyarwanda pamoja na nchi nyingine ambako wataipeleka hivi karibuni.