Msanii Ndefu Baiso

Patana na msanii wa bongofleva Ndefu Baiso ambaye ni mdogo wake Madee

Muziki wa bongofleva umeendelea kupata wageni, sasa hivi ni huyu mdogo wake Madee, ni mtoto wa mwisho kwenye familia yao ya watoto nane.

Anaitwa Ndefu Baiso, alianza muziki akiwa na miaka 14 tu na ikatokea kaupenda sababu ya mazingira ya nyumbani yaliyokua yametawaliwa na muziki wanaoufanya kaka zake.
 
Kutana na msanii mwingine Korede Bello, aliyeanza muziki wake akiwa mdogo, kwenye #Ginjah Jumamosi saa 23:00 kwenye MTV Base.
 
Baba yake mzazi kakiri kwamba kwa miaka mingi amekua akiwasaidia au kuwapa support watoto wake ambao ni Madee ambaye alimlea na marafiki zake wa kundi la Tiptop na sasa ni zamu Ndefu.

Ndefu ana umri wa miaka 19 tu na ameachia single yake ya kwanza inaitwa Gusa Unate ambayo kasimama mwenyewe. Kazi imefanyika kwenye studio yao nyumbani na kaamua kuisimamia mwenyewe alafu baadae mwakani ndio zitafuata kolabo na kaka yake Madee.

Ndefu alimaliza form IV mwaka 2014 Dar es Salaam na hatarajii kuendelea kusoma sababu anaamini kipaji chake kinaweza kumfikisha mbali kuliko darasa ambalo amekua akiling'ang'ania lakini hajawa na bahati ya kufaulu.

Related