Mteuliwa wa AMVCA BOKBO MOVIE

Kutana na Godliver Gordian, muigizaji aliyepata tuzo kama Best Actress kwenye role yake ya Aisha kwenye bongomovie la Aisha mwaka 2016. Mwanadada huyu amekuwa kwa kasi sana kutokana na kazi nzuri anayoifanya kwenye filamu za Kitanzania na pia amecheza kwenye bongomovie la Homecoming na pia kwenye tamthilia ya Siri ya Mtungi.

Filamu hizi mbili za Aisha na Homecoming pamoja na tamthilia Siri ya Mtungi zote zipo kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards 2017.

Pata orodha yote ya wateuliwa wa AMVCAs 2017 hapa.

Kwenye hii video hapa chini, Godliver ameelezea kiufupi historia yake ya uigizaji na kuomba kura kwa bongomovie hizo tatu ili waweze kunyakua tuzo za AMVCAs 2017. Msikilize.

 

Wewe kama shabiki usikose kupigia filamu hizo za Kitanzania kura. Tarehe 24 Februari ndiyo siku ya mwisho ya kupiga kura, kazi kwako!

Mengi ya bongomovies, usikose kutazama filamu Jirani siku ya Alhamisi 9 Februari saa 14:00 EAT.