Msanii wa South Africa KO

Msanii wa South Afrika awasili Dar es Salaam kwa media tour

Rapper maarufu kutoka South Africa K.O (Mr. Cashtime) ambaye jina lake limetajwa sana kwenye ardhi ya Tanzania kutokana na hit single aliyoshirikishwa na Vanessa Mdee, amewasili Dar es Salaam Jumapili.

Ungana na K.O na Vanessa Mdee kwenye single ya Nobody But Me kwenye Hitlist, Jumapili 23 August saa 23:00 kwenye Maisha Magic East.

Mr. Cashtime atakuwepo kwenye jiji hili kwa siku kadhaa kwa ajili ya media tour upande huu wa Tanzania ambao hata nyimbo zake nyingine zimeanza kupata airtime.
 
Baadhi ya vitu anavyotarajiwa kuvizungumza ni pamoja na kolabo na Wabongo na ishu zake nyingine zinazohusu muziki wake.
 
Kwenye exclusive na dstv.com kwenye red carpet ya MAMAs 2015, K.O alisema amefurahishwa sana na mapokezi ya Watanzania na anatarajia siku moja atapata nafasi ya kusikika zaidi sababu anaukubali muziki pia wa Tanzania.
 
Hit single ya 'Nobody But Me' aliyoshirikishwa na Vanessa Mdee ilifanya vizuri kwenye chati za muziki mbalimbali Afrika zikiwemo za South Africa na Nigeria, nyumbani Tanzania pamoja na Kenya lakini muziki wa V Money umeendelea kuwa mkubwa pia kwenye nchi kama Rwanda na Burundi.