ali kiba, Neyo na wasanii wengine kwenye coke studio

Kiba alimkaribisha Ne-Yo hapa Nairobi katika Coke Studio Africa.

King Kiba kutoka Tanzania, aliyetuletea nyimbo kama Mwana na Chekecha Cheketua alikutana na mwanamuziki maarufu toka Marekani, Ne -Yo, anayejulikana kuwa mwanamuziki na mwandishi wa muziki moto moto kama Let me love you, Sexy Love and Miss Independent.

Kiba alimkaribisha Ne-Yo hapa Nairobi katika Coke Studio Africa.

Ali Kiba na baadhi ya wanamuziki wengine kama Wangechi (Kenya), Dama Do Bling (Mozambique), Ice Prince (Nigeria) na Maurice Kirya (Uganda) walijadiliana na Ne-Yo kuhusu muziki wa Afrika ambao alikubali unapata umaarufu kote duniani. Ilisemekana Kiba na Ne-Yo wanamatumaini ya kushirikiana haswa katika kuandika na kurekodi nyimbo mpya pamoja.

Jiunge na wasanii wengine maarafu kutoka East Afrika kwenye Hitlist, Jumapili 23 August saa 11:00 kwenye Maisha Magic East.

King Kiba pia anatarajiwa kurekodi wimbo na wanamuziki  hao katika mfumo mpya wa Coke Studio Africa msimu wa 3, utakaozinduliwa mwezi wa Oktoba mwaka huu. Hii ni mara ya kwanza ya Kiba kushiriki kwenye Coke Studio ambapo ameshirikiana na msanii wa Kenya Victoria Kimani katika nyimbo za mash-up.

Tunamkaribisha Ne-Yo huku Afrika Mashariki!