Msanii Ndanda Kosovo

Weekend iliyopita Tanzania na muziki wa dance zilipata msiba wa staa wa siku nyingi kwenye muziki huu, Ndanda Kosovo ambaye alifariki hospitalini Muhimbili kutokana na ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

Mipango ya mwanzoni ilikua ni Ndanda asafirishwe kwenda kuzikwa kwao Congo DRC lakini taarifa zilizotolewa na mjomba wake zinasema mipango imebadilika.
 
Mengi ya watanzania na maisha yao pia unaweza kuitazama kwenye Inside Bongowood, Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Kumbe Ndanda Kosovo alishawahi hata kumwambia waziri wa michezo Nape Nnauye kwamba akifa anataka azikwe Tanzania alikokaa kwa zaidi ya miaka 20 na sio Congo DRC.
 
Maziko yake ni Jumatano April 13 Dar es Salaam na mpaka Jumanne April 12 mama yake mzazi alikua akitarajiwa kuwasili kutoka Congo DRC.
 
Ndanda Kosovo ni jina lililokua kubwa kwa miaka mingi nchini Tanzania kupitia single kadhaa kama Chocolate, Jela na nyingine nyingi.