Msanii Dogo Janja kutoka Tanzania

Kidebe ya Dogo Janja yaweka record youtube

Dogo Janja ni miongoni mwa wasanii wa bongofleva ambao wako kwene industry wakiwa na umri mdogo na kuanza mziki wakiwa wadogo sana na anafanya vizuri kwa sasa hivi na hit song yake Kidebe.

Kutana na Dogo Janja na hit yake ya Kidebe kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160).
 
Hit maker huyu ameonesha furaha yake baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya Kidebe kuweka record yake ya kufikisha 1 million viewers sasa hivi.
 
Aliandika, “The best is still yet to come.. #1MillionViews #Kidebe Directed By @hanscana_ Cc: @babutale @madeeali @tundamantz #HipHop.”
 
Hii ni video ya kwanza ya Dogo Janja kutazamwa zaidi katika mtandao huo ambapo mpaka Jumatatu hii imeshatazamwa mara 1,001,982 tangu ilipotoka miezi mitano iliyopita.

 Nayo video yake ya My Life inaonekana kusogea japo ndio ya kwanza kutoka kabla ya Kidebe ambapo mpaka sasa imeshatazamwa mara 866,210 YouTube.